TANZANIA - #likelafargeholcim

For building tips and information, follow us on

Kampuni ya LafargeHolcim Group

LafargeHolcim ni kampuni inayoongoza katika utengenezaji wa bidhaa na utoaji huduma za ujenzi ambayo imefanya kazi katika masoko ya kimataifa kwa miongo kadhaa. LH hutengeneza saruji, kusaga kokoto na kuandaa zege lililochanganywa tayari kwa ajili ya miradi ya ujenzi, kuifaa miradi midogo ya nyumba za makazi na pia miradi mikubwa ya miundombinu kama vile maghorofa, mabwawa, madaraja na barabara.

Kampuni ya LafargeHolcim, iliyo na makao yake makuu nchini Uswisi, inafanya kazi katika nchi zaidi ya 80 ina viwanda zaidi ya 2300 zinazofanya kazi, na ina wafanyakazi 90,000. Tumetoa leseni za hatimiliki na maombi ya leseni za hatimiliki 2000 za huduma zetu bunifu za ujenzi.

Historia ya LafargeHolcim

Kampuni hii ilianzishwa Julai 2015 wakati Lafarge, kampuni ya viwanda iliyosifika kwa utengenezaji saruji, kokoto , jasi, na zege lililochanganywa tayari, ilipoungana na Holcim, kampuni ya saruji ya Uswisi. Kampuni hii mpya ilizinduliwa rasmi duniani kote chini ya jina la LafargeHolcim.

Lafarge ilianzishwa mwanzoni mwaka 1833 nae Bw. Joseph-Auguste Pavin de Lafarge nchini Ufaransa kwa lengo la kuchimba chokaa katika eneo la Mont Saint-Victor lililokuwa na chokaa . Bidhaa hii hutumiwa kutengeneza chokaa inayoimarishwa kwa maji na hutumiwa kama kiungo msingi cha kukausha saruji.

Utafiti na ustawi katika kampuni ya LafargeHolcim

Kampuni hii ilianzisha kituo cha kwanza cha utafiti na ustawi (R & D) kwa sekta ya ujenzi na imewekeza mamilioni ya Euro katika R&D miaka kadhaa iliyopita. Hii inamaanisha kuwa LafargeHolcim inazalisha bidha, ufumbuzi na huduma bunifu zaidi katika sekta ya ujenzi.

Baadhi ya mafanikio yetu ya R&D ni pamoja na kupunguza gharama za ujenzi, kupunguza bei za
nyumba, kuboresha uwezo wa majengo, kuokoa nishati, kutengeneza viungo vipya vya saruji, kupunguza uharibifu wa mazingira na kufanya vituo vya kufanyia kazi viwe bora kwa wafanyakazi wote. LafargeHolcim itatabiri mitindo na matumizi ya teknolojia mpya kila mara ili iendelee kuwa kampuni ya kisasa.

Afya na usalama katika LafargeHolcim

Kuzuia ajali kwenye maeneo ya kazi zetu ni jambo muhimu kwetu, lakini lengo letu kuu ni kuhakikisha hakuna mfanyakazi yeyote anayejeruhiwa katika vituo vyetu vyote. LafargeHolcim inajitahidi kudumisha mazingira salama na yanayotunza afya ya wafanyakazi wote, makandarasi, jamii na wateja.

Tunadumisha mfumo wa kimataifawa usimamizi wa afya na usalama ili kuendeleza historia yetu
ya usalama. LafargeHolcim huendelea kujaribu kuboresha historia hii kwa kudhibiti kikamilifu vihatarishi vyote katika nyanja mbalimbali za biashara yetu.

Mafunzo na ushirikishwaji hudumisha nidhamu ya ufanyakazi na kuweka maadili ya kudumisha usalama miongoni mwa wafanyakazi. Wadau wote huelezwa waziwazi kuhusu masuala yoyote ya afya na usalama yanayotambulika ili kuwahamasisha kuhusu hatari zilizopo.

Mkakati wa 2022

Mkakati wetu wa miaka ijayo ni kufanya ujenzi unaoleta ustawi. Lengo la kampuni ya LafargeHolcim ni kuwezesha ustawi wenye faida kwa kurahisisha taratibu za biashara na kuwawezesha washikadau kupata faida endelevu.

Tumeanzisha Mkakati wa 2022 unaoambatana na uwezo wetu kama kampuni. Mkakati huu utasababisha ustawi katika kiwango cha juu katika miaka michache ijayo. Soko la kimataifa la nyenzo za ujenzi linatabiriwa kukua kwa asilimia mbili hadi tatu kila mwaka. LafargeHolcim itatumia nafasi hii ya ustawi kujitahidi iwe na utendaji bora kuliko utendaji wastani wa sokoni.

LafargeHolcim itatumia rasilimali zake nyingi kuwekeza katika masoko yanayokua. Kampuni hii imezindua idara mpya ya biashara inayojulikana kama Huduma na Bidhaa, ambayo inawahudumia.wateja kwa njia bora zaidi. Idara hii ya biashara kwa sasa hutoa bidhaa za zege zilizotengenezwa awali, lami, chokaa na huduma za ukandarasi.

Mkakati wa urahisishaji na utendaji unajumuisha kutumia mbinu ya gharama nafuu zaidi inayofuata muundo rahisi zaidi wa kishirika. LafargeHolcim pia itazingatia zaidi kwa kanuni za utendajiza husika na masoko yake.

___

Je, wajua, LafargeHolcim ilitoa saruji na kokoto iliyotumika kujenga viwanja vya Kombe la Dunia la FIFA la 2010 nchini Afrika Kusini; Uwanja wa Cape Town mjini Cape Town, Uwanja wa Nelson Mandela Bay mjini Port Elizabeth, Uwanja wa Peter Mokaba mjini Polokwane, Uwanja wa Mbombela mjini Nelspruit na Uwanja wa Moses Mabhida mjini Durban.

___

LafargeHolcim Tanzania imekuwa ikiitengenezea nchi hii na mataifa jirani bidhaa yetu ya saruji ya Tembo, ambayo ni ya kiwango cha kimataifa, kwa zaidi ya miaka 30. Ofisi yetu ya kuu na kiwanda jumuisha kikamilifu zipo Songwe, Mkoa wa Mbeya, Kusini Magharibi mwa Tanzania.

___

Katika kampuni ya LafargeHolcim Tanzania, tunawapa wateja kipaumbele. Tunasikiliza mahitaji yao maalum ili kuwahudumia na kuwatolea bidhaa bora zaidi zinazokidhi mahitaji yako. Unaweza kututegemea sisi kama kiongozi mpya wa utengenezaji nyenzo za ujenzi na uwezo wetu wa utafiti na ustawi ambao umepelekea utengenezaji wa nyenzo bora zaidi za miradi yao ya ujenzi, iwe mikubwa au midogo.

___

Tufuate kwenye Facebook, Twitter, Instagram na Pinterest upate vidokezo vya kisasa kuhusu mbinu za miradi ya kujifanyia mwenyewe na habari za kisasa kuhusu sekta ya ujenzi. Angalia kituo chetu cha Instagram upate ufahamu zaidi kuhusu kazi tunayoifanya na jumuiya za karibu na viwanda vyetu na jinsi tunavyoyatunza mazingira asili.

Synthetic fibres can increase the durability of concrete

Contractors sometimes add synthetic fibres to their concrete mix. These fibres of man-made polymers are specifically engineered to withstand the long-term alkaline environment within a concrete mix. They are used to minimise cracking, lower the permeability of the concrete and increase the strength of the structure. They act as a secondary reinforcement element; the primary …

The eight types of construction company

There are many different types of construction company. Not all contractors specialise in the same fields and not all companies do the same construction work. Depending on the type of work they do, construction companies can be classified into the following eight types: 1. General contractors A general contractor provides all of the labour, equipment, …

How to fix common concrete slab problems

When working with concrete, contractors may encounter a few different problems. The following issues can sometimes occur when pouring concrete slabs. While some aspects of working with concrete slabs have changed over the years, many issues have not. Here are three common problems that come with pouring concrete slabs, and their possible solutions. 1) Excessive …

The importance of having a schedule for a construction project

Construction projects are delicate operations that need to run on time in order to stay within the allocated budget. As soon as a project is delayed, it costs the contractors and building owners more money. Having a strict schedule is important as it keeps the project on time and allows all workers to know when …

How to prepare a concrete surface for a topping

Sometimes concrete surfaces are given a decorative topping that adds further protection and durability to a floor or carpark. The underlying concrete will need to be prepared properly before any topping is laid on top. This will ensure that a good bond is formed between the two materials and that no cracks or chips will …